Sunday 8 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA PILAU YA NYAMA YA NG'OMBE

                     MAHITAJI
  -Mchele 
  -Nyama ya ng'ombe
  -Viazi mbatata(mviringo)(potato)
  -Vitunguu maji(onions)
  -Vitunguu swaumu(garlic)
  -Tangawizi iliyosagwa(ginger)
  -Karafuu(cloves)
  -Pilipili manga(Black pepper)
  -Chumvi(salt)
  -Binzari nyembamba nzima(cumin seed 1/2 kijiko cha cahi)
  -Binzari nyembamba ya kusaga 1 kijiko cha chai
  -Mafuta(vegetable oil)
  -Limao
  -Pilipili(chilli)
  -pilipili hoho(green pepper)
  -Nyanya(fresh tomato)

                               HATUA ZA KUPIKA
   -Katakata ya nyama yako kulingana na saizi uitakayo mwenyewe
   -Chemsha ya nyama yako na pia weka limao, Tangawizi pamoja na chumvi.
   -Wakati inaendelea kuchemka nyama yako, loweka sasa mchele wako katika maji.
   -Menya viazi vyako, pia katakata vitunguu vyako pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni kwa ajili         ya baadae
   -Weka sufuri yako jikoni na uweke mafuta yako ya kupikia,baada ya mafuta kupata moto weka vitunguu vyako ( na vitunguu maji) na uvikaange mpaka viwe rangi ya kawia(brown)
   -Baada ya hapo weka nyama yako nayo ikaange mpaka iwe rangi ya kawia (brown), baada ya hapo weka kitunguu swaumu na tangawizi tena kidogo na uikoroge vizuri na uiache ili ikaangike kwa muda wa dakika 2 au 3
-Baada ya hapo weka spices(viungo) ambavyo ni Binzari nyembamba ya unga, karafuu, amdalasini, hiriki, pilipili manga pamoja na viazi mbatata(mviringo),baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mchanganyiko huo mpaka uchanganyike vizuri 
-Baada ya hapo weka mchele wako na ugeuze geuze ili uchanganyike na viungo 
-Baada ya hapo weka chumvi kwa kiasi sana na uweka maji yako yale ya moto ya kutosha na ukoroge na baada ya hapo funika na uchemke kwa moto wa wastani.Pindi maji yanakaribia kukauka weka Binzari nyembamba nzima na ufunike uchemke mpaka maji ya kauke.Maji yakisha kauka ugeuze na ufunike mpaka uive
                     MAANDALIZI YA KACHUMBARI
  -Katakata vitunguu katika bakuli na uweke chumvi na maji na vioshe kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu na uvioshe mpaka chumvi itoke
 -Baada ya hapo osha nyanya, pilipili hoho na ukatekate slice nyembamba na uchanganye katika vitunguu pia kamulia limao  na uweke chumvi pia unaweza weka pilipili kama ukipenda..........!!!!!!!!!!!!

NAWATAKIA CHAKULA CHEMA...............!!!!!!!!

AHSANTENI SANA WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON


  
  
        

  

3 comments:

  1. Naomba utufundishe fricassee de poulet a l'ancienne na tui.

    ReplyDelete
  2. ucjari nitaandaa bila wasiwasi nipo kwaajili yenu wangu

    ReplyDelete