Monday 17 February 2014

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA MCHUZI WA NYAMA AU BEEF STEW

           
                  MAHITAJI
        - Nyama ya ng'ombe (Beef)
        - Soy sauce
        -Vitunguu (onions)
        -Mafuta ya kula( vegetable oil)
        -vitunguu swaumu(garlic)
        - Pilipili hoho(green pepper)
        - Karoti(carrot)
         -Pilipili manga(black powder)
         - mchuzi wa nyama(beef stock or beef broth)
         -Nyanya ya kusaga(Tomato paste)


                   HATUA ZA KUPIKA
          -Katakata nyama kwa mkato wa pembe nne(cubes)
         - Chemsha nyama yako mpaka iive kabisa na vitunguu swaumu
         -Katakata karoti, pilipili hoho, pamoja na vitunguu kwa mkato wa julieni
         -Baada ya nyama yako kuiva weka pembeni na uweke flampeni weka mafuta kiasi kidogo sana
         - Baada ya mafuta kupata moto weka vitungu, pilipili hoho pamoja na karoti na uanze kuangaa(sautee)
         -Wakati naendelea kukaanga weka soy sauce
         -Baaada ya kuiva mbogamboga zako(karoti, vitunguu na pilipili hoho) ipua na uweke pembeni
         -Baada yapo chukua nyama yako ambayo uliichemsha na uichuje na ule mchuzi wako utunze kwaajili              ya baadae.
         -Baada ya hapo chukua nyama flampeni na uweke mafuta kidogo na uikaange
         - Baada ya hapo weka zile mbogamboga zako(karoti, pilipili hoho na vitunguu) yaani uchanganye                     pamoja na nyama yako
         -Baada ya kuchanya mbogamboga zako, weka soy sauce
         -Baada ya hapo weka nyanya yako ya kusaga(tomato paste) na uikologe au kuichanganya pamoja
         - Baada ya weka mchuzi wako uliouchuja kutoka ktk nyama, au mchuzi wa nyama(beef stock or broth
         - Baada ya hapo weka pilipili manga,na chumvi(black pepper and salt)
         -Baada ya hapo punguza moto wako na uiache kwa muda wa dakika 5 tu na uipue
         - Chakula hichi unaweza ukala na wali(rice)
         -Mwishooooooooo

AHSANTEN SANA WADAU WANGU.........!!!!!
 NAWATAKIA CHAKULA CHEMA WAPENDWA............!!!!!!!


ANGALIA HII PICHA...!!!!