Sunday 22 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA KUSAGA PAMOJA NA UNGA WA MIKATE(MASHED POTATO WITH BREAD CRUMB)

 Mahitaji
    -Viazi mbatata(mviringo)
    -Cream au maziwa
    -Spreadable cheese(philadelphia)
    -Kitimiri(coriender)
    -Majani ya laurusi (bay leaves)
    -Mayai
    -Unga wa ngano
    -Unga wa mikate

         Jinsi ya kuandaa sasa
    -Menya viazi na uvikate kate
    -Chopchop kitimiri(coriender)
   
          Hatua za kupika
    -Chemsha viazi,chumvi pamoja na majani ya laurusi(bay leaves), chemsha mpaka vilainike ili uweza kuviponda kwa baadae. Baada ya kuiva kwa viazi viipue na kuchuja maji na hatimaye weka sufuria yako tena jikoni na uweke viazi vyako ambavyo ulivichuja hapo awali.Na uanze kuvisaga sasa.
    -Wakati unaendelea kuvisaga viazi vyako unatakiwa kuweka sasa Cream au maziwa,Spreadable cheese pamoja na kitimiri(coriender) huku unaendelea kuvisaga viazi yako.
    -Endelea kusaga viazi vyako kwa muda wa dakika 5, na hatimaye vitakuwa vimesagika na kuiva kabisa.
    -Baada ya hapo chukua viazi vyako na utengeneze shepu kama kibomba.
    -Baada ya hapo pasua mayai yako na uweke katika bakuli kubwa kidogo, na uweka unga wa ngano ktik bakuli yake kubwa nayo pamoja na unga wa mikate nayo .
    - Baada ya kutengeneza shepu yako kama ya kibomba, chukua sasa na uweke katk unga wa ngano, na uweke katika mayai na mwisho katika unga wa mikate na uifadhi pembeni utafanya hivyo mpaka utakapo maliza viazi kwa jinsi ulivyo vishepu umetoa vingapi.
   -Weka flampeni yako jikoni na mafuta kiasi ili ukaange sasa(shallow fry)   
   -utakaanga mpaka utapoona rangi ya brown.
   -Na hapo vitakuwa tayari unaweza ukala na sosi (sauce) yako.
 NAKUTAKIA CHAKULA CHEMA MPENDWA WANGU.........!!!!!!!!
 AHSANTENI SANA WADAU WANGU.............!!!!!!!!!
Hapa vikiwa katika unga wa mikate
Hapa umetengeneza ktk shepu na umeweka ktk mayai

 BY IRON CHEF JACKSON
   

Hapa unakaanga sasa
Hapa tayari kwa kuliwa sasa

No comments:

Post a Comment