Saturday 14 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA KEKI YA UNGA WA MAHINDI

                  MAHITAJI
   -Unga wa mahindi 250g
   -Unga wa ngano 200g
   -Sukari 250g
   -Baking powder 10g
   -Vanila essence 1 kijiko cha chakula
   -Eggs 9(75g)
   -Cream au maziwa
   -Siagi(butter)


              HATUA ZA KUPIKA 
   -Unga wa mahindi pamoja na unga wa ngano changanya pamoja na uchekeche.
   -Weka sukari pamoja na siagi na uchanganye pamoja na uiweke katika mashine ya kuchanganyia
   -Ya vunje mayai yako na uweke vanila yako katika maya.
   -Chukua unga wako uliouchekecha na uweka baking powder
   -Weka mayai yako ambayo ndani yake kuna vanila na uchanganye pamoja katika mchanganyo wako siagi na sukari ikiwa ndani ya mashine ya kusagia na baada ya kuchanganyika unatakiwa uutoe huo mchanganyiko wako katika mashine.
   -Chukua unga wako( unga wa mahindi+ unga wa ngano+Baking powder) na uweke kidogo kidogo katika mchanganyiko wako ule wa (Siagi, Sukari, Mayai ambayo ndani yake kuna vanila) huku unakoroga utaendelea hivyo mpaka utakapoona imekuwa nzito nzito.....!!
  -Baada ya hapo utandaze katika baking tray yako na uweke katika oveni yako
  -Utaona rangi yake na kuwa kama ya njano..........!!!!!!
  -MWISHOOOOOOOOOO

NAKUTAKIA KEKI NJEMA UONJAPO.........!!!!!!!!!!

AHSANTENI SANA WADAU WANGU..........!!!!!!!!!!!
  
BY IRON CHEF JACKSON
   


   

No comments:

Post a Comment