Thursday 13 August 2015

KARIBUN TUJIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA MARBLE KAKE

Hii inaliwa na watu                   6 - 8
Muda wa maandalizi ni dakika      15
Muda wa kupika                             50


MAHITAJI
- Mayai 3
- Siagi 3/4 kikombe
- Chumvi pinch
- Unga wa ngano  1 -1/3 vikombe
- Baking powder 1 kijiko kimoja cha chai
- Sukari  1 kikombe
- Cocoa powder 1/2



JINSI YA KUPIKA

  1. Vunja mayai yako na utenge viini pamoja na utete, yeyusha siagi yako. Changanya utete wa mayai yako pamoja na chumvi na unachanganye vizuri, na baada ya hapo chukua unga wako wa ngano na uchangaye na baking powder pamoja.
  2. Chukua Siagi yako uliyeyusha na uchanganye na sukari yako, baada ya hapo changanya pamoja na viini vya mayai na uendelee kuchanganya.
  3. Chukua unga wako wa ngano ambao uliuchanganya pamoja na baking powder na uchanganye ktk ule mchanganyiko wako wa siagi, sukari na viini vya mayai.
  4.  Baada ya hapo changanya na ule uteute wa mayai ambao unamchanganyik wa chumvi u fold pamoja.
  5. Washa oven yako nyuzi joto 400F
  6. Chukua ule mchanganyiko wako na uugawe ktk sehem mbili,.
  7. Baada ya kugawa mchanganyiko ktk mabakuli, basi bakuli moja wapo changaya na cocoa powder.
  8. Baada ya hapo paka baking tray yako siagi kidogo
  9. Baada hapo weka mchanganyiko wako kwa awamu yaani, utaanzaa labda kuweka mchanganyiko ambao hauna cocoa powder kidogo ktk baking tray then utaweka na ule mchanyiko amabao hauna cocoa powder, hutafanya hivyo kidogo kidogo mpaka baking tray yako itakapo kuwa full na baking tray ni moja michanganyiko yote miwili ktk baking tray moja



KARIBUNI SANA 


BY 

IRON YOUNG CHEF JACKSON

Wednesday 12 August 2015

                                        JINSI YA KUPIKA TOMATO SAUCE
- Hii ni sauce ambayo utokana na nyanya kupitia tomato sauce unaweza kudhalisha sauce mbali mbali kma vile
  - Chill sauce
  - Arrabiata sauce
  - Boleness sauce n.k


Mahitaji
- Nyanya
- Vitunguu maji
- Vitunguu swaumu
- Leeks
- Sukari kijiko cha kimoja cha chai
- Tomato paste
- Tangawizi
- Maji au vegetable stocka
- Mafuta ya kupikia
- Corriender
- Chumvi


                      JINSI YA KUANDAA
1: Osha nyanya zako na ukate kwa style uipendayo, na uweke kwenye chombo kisafi.
2: Osha vitunguu maji na uchopped pamoja na leeks
3: Blend vitunguu swaum pamoja na tangawizi
4: Chopped corriender(kotimiri)


                      JINSI YA KUPIKA

  1. Weka sufuria yako jikoni na uweke mafuta yako kidogo ya kupikia.
  2. Weka vitunguu maji pamoja na vitunguu swaum na tangawizi ulivyo blend na uweke na leeks pamoja na kotimiri
  3. Baada ya hapo weka nyanya zako na ukoroge koroge na uache mpaka nyanya ziive na uweke maji yako kiasi.
  4. Baada ya hapo uweka tomato paste yako, na uendelee kukoroga kidogo.
  5. Weka chumvi pamoja na sukari na ukoroge na uiche kwa muda wa dakika 5 na uzime ujiko.
  6. Baada ya hapo chukua na uiblend na huo mchuzi utakao patikan ndio sauce yenyewe.


NOTE
Kupitia sauce hiyo unaweza kupikia chakula chochote upendacho kam TAMBI, BEEF, CHICKEN, N.K



KARIBUNI SANA


BY

IRON YOUNG CHEF JACKSON