Wednesday 18 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA WALI WA MAYAI KWA STAILI YA KICHINA( FRIED RICE CHINESS)

            MAHITAJI
  -Mchele
  -Mafuta( vegetable oil)
  -Soy sauce
  -Chumvi (salt)
  -Pilipili hoho (green pepper)
  -Karoti (carrot)
  -Maji ya moto (hot water0
  -Kuku(fillet chicken or breast chicken)
  -Vitunguu (onions)
  -Mayai
  - Siagi au blue band

                        HATUA ZA KUPIKA 
   -Diboni kuku wako( ondoa mifupa na ubakiwe na steki tu ya kuku), na ukatekate mkato wa julieni.
   -Katakata pilipili hoho,Karoti kwa mkato wa julieni.
   -Chopchop vitunguu vyako vyote.
   - Kaanga mayai yako na ukate julieni.
   -Chemsha maji yawe yamoto na uweke pembeni.
   -Osha mchele wako na uweke pembeni.
   -Weka sufuria yako jikoni pamoja na mafuta yako. Baada ya mafuta kupata moto weka vitunguu vyako.
   Baada ya vitunguu kuiva, weka mchele wako na ukaange kwa muda kidogo na uweke chumvi.
   -Baada ya kuukaanga mchele wako, weka maji yako yale ya moto na uufunike sasa.
   -Wakati sufuria yako ipo jikoni, chukua flampeni yako na uweke siagi au blue band,
   - Baada ya kuyeyuka blue bandi yako au siagi yako, weka karoti, hoho pamoja na kuku wako ambao ulidiboni(fillet) na ukaange(shallow fry)  pamoja na uweka soy sauce yako.
   - Baada ya kuiva huo mchanganyiko wako(kuku, hoho na karoti) weka pembeni sasa.
   -Baada ya wali kukaribia kuiva changanya huo mchanganyiko wako wa (kuku, hoho na karoti) pamoja na mayai yako weka pamoja katika wali na uchanganyi pamoja ili uchanyike, baada ya hapo ufunike kwa muda kidogo na utakuwa umeiva 
   - Sasa chakula tayari kwa kuliwa na kwenda mezani sasa

NAWATAKIA CHAKULA CHEMA..........!!!!!!!
 AHSANTENI SANA WADAU WANGU.........!!!!!!!!
 NAWATAKIA PIA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA............!!!!!!!!

BY IRON CHEF JACKSON
MAYAI MKATO WA JULIENI
  
KUKU AMEKATWA MKATO WA JULIENI
KAROTI NA HOHO ZIMEKATWA MKATO WA JULIENI
CHAKULA TAYARI KWA KULIWA

No comments:

Post a Comment