Thursday 12 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA SUPU YA DENGU

                         MAHITAJI

       -Unga wa dengu(Lentts flour)
       -Mchuzi wa kuku(Chicken stock)
       -vitunguu maji(onions)
       -vitungu swaumu(garlic)
       -Majani ya vitunguu(leaks)
       -Majani ya kitimiri(coriender)
       -Chumvi(salt)
       -Pilipili manga
       -Siagi
                    HATUA ZA KUPIKA
       -Katakata(chopchop) vitunguu, vitunguu swaumu, majani ya vitunguu,majani ya kitimiri.
       -Chukua unga wa dengu pamoja na mchuzi wa kuku(chicken stock) changanya pamoja na uupige na whipped wakati unauchanganya.
      -Weka sufuria yako jikoni pamoja na siagi
      -Baada ya siagi kupata moto weka vitunguu maji,majani ya vitunguu, vitunguu swaumu,pamoja na majani ya kitimiri na ivikaange pamoja mpaka vieve pamoja.
      -Baada ya kuiva hivyo viungo, weka ule mchanganyiko wako wa mchuzi wa kuku(chicken stock)pamoja na unga wa dengu.
Baada ya hapo, weka chumvi pamoja na pilipili manga na uiache kwa muda ili ichemke na upunguze moto wako.
 -Baada ya hapo unatakiwa uiblendi katika blenda
 -Endapo ikaonekana nzito sana unatakiwa uongeze mchuzi wa kuku(chicken stock) au maji.
Na hapo supu yako itakuwa imekamilika

NAKUTAKIA CHAKULA CHEMA

AHSANTENI SANA WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON
 Hapa imekwisha iva tayari













Hapa tayari kwa kuliwa kabisa

No comments:

Post a Comment