Monday 2 December 2013

KARIBU TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA KUSAGA (MASHED POTATOES)

Viazi vya kusaga ni chakula kitamu sana ambacho kimebeba asilimia kubwa ni Wanga pamoja na Proteni, chakula hichi kinafaida kubwa katika miili yetu kama vile kujenga mwili(shape of the body), kuupa mwili nguvu(to be strong of the body).Pia chakula hichi huwa kina wafaa watoto wadogo miaka 2 na kuendelea , pia kina wafaa sana wakina mama wajazito pamoja na wazee kwa ajili ya afya zao ktk mili yao.
                     
                                 TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA SASA

          Mahitaji
    -Viazi mbatata(mviringo)
    -Cream au maziwa
    -Spreadable cheese(philadelphia)
    -Kitimiri(coriender)
    -Majani ya laurusi (bay leaves)

         Jinsi ya kuandaa sasa
    -Menya viazi na uvikate kate
    -Chopchop kitimiri(coriender)
   
          Hatua za kupika
    -Chemsha viazi,chumvi pamoja na majani ya laurusi(bay leaves), chemsha mpaka vilainike ili uweza kuviponda kwa baadae. Baada ya kuiva kwa viazi viipue na kuchuja maji na hatimaye weka sufuria yako tena jikoni na uweke viazi vyako ambavyo ulivichuja hapo awali.Na uanze kuvisaga sasa.
    -Wakati unaendelea kuvisaga viazi vyako unatakiwa kuweka sasa Cream au maziwa,Spreadable cheese pamoja na kitimiri(coriender) huku unaendelea kuvisaga viazi yako.
    -Endelea kusaga viazi vyako kwa muda wa dakika 5, na hatimaye vitakuwa vimesagika na kuiva kabisa. 
Hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa, pia chakula hiki kina faa kuliwa sana na nyama choma(Grilled beef) ....!!!!!! 
Nawatakia chakula chakula chema 


   
    
   
     

6 comments:

  1. Safi sana, wangu. Watu wakizoea upishi huu wataweza kujaribu viungo vingine, kama vile labda majani mengine. Nakutakia kila la heri katika blogu hii.

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa kutupatia blogu nzuri ambayo tunaamini tutajifunza mambo mengi......mungu akubariki

    ReplyDelete
    Replies
    1. ahsante sana JOHN B karibu kwenye blog ya misosi, uliza unachojickia chochote

      Delete
  3. Tulia baba. Nipo tayari kwa hiyo kazi ya kuonja chochote! Sija-install condenser kwenye mdomo wangu, lakini, hamna shida.

    ReplyDelete
  4. hahahahahahahahahahahah......!!! Basi nitakuajiri kwa kazi ya kuonja tu misosi tu kaka

    ReplyDelete