Monday 30 December 2013

JE UNAJUA VYAKULA GANI WANAOKULA WAFUGA RASTA(DO YOU KNOW THE KIND OF FOODS WHO ARE EATING VEGETARIAN)

                                WAFUGA RASTA(VEGETARIAN PEOPLE)
Hawa ni watu ambao wasio kula nyama ya aina yeyote, kutoka na imani walizonazo kwa mfano, imani za kidini kwa wenzetu wahindi huwa hawali nyama ya ng'ombe wakiamini ndie muumba wao, pia wat hawa huwa hawapendi wakimuona myama anachinjwa au kuona damu ya mnyama.

                                       AINA ZA WAFUGA RASTA
   Hawa wafuga rasta wamegawanyika katika makundi mawili(2) ambayo ni
        -Kuna wafuga rasta wasio kula nyama kabisa
        -Kuna wafuga rasta wasio kula nyama na hata kile kinachodhalishwa na mnyama .

                         WAFUGA RASTA WASIO KULA NYAMA
Hili ni kundi la wafuga rasta wasio kula nyama kabisa, hivyo kundi hili huwa wanakula vyakula vinavyodhalishwa na mnyama kwa mfano, maziwa, mayai n.k 

       AINA ZA VYAKULA WANAVYOKULA WAFUGA RASTA WASIO KULA NYAMA
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula wanavyokula wafuga rasta wasiokula nyama tu, ambayo ni
        -Maziwa(milk)
        -Mayai(eggs)
        -Mbogamboga za majani(vegetables)
        -Tambi(pasta)
        -Wali(rice)
Hivyo ni baadhi ya vyakula wanavyokula kundi hili la wafuga rasta wasio kula nyama.

WAFUGA RASTA WASIO KULA NYAMA HATA KINACHODHALISHWA NA MNYAMA
Hili ni kundi la wafuga rasta ambalo hawali nyama wala anachaodhalisha mnyama kwa mfano nyama, mayai, maziwa n.k hivyo vyakula jamii ka hii huwa hawali kabisa.

AINA ZA VYAKULA WANAVYOKULA WAFUGA RASTA WASIOKULA NYAMA HATA KINACHODHALISHWA NA MNYAMA
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula wanavyokula aina hii ya wafuga rasta ambavyo ni
      -Mbogamboga za majani(vegetable)
      -Wali(rice)
      -Tambi(pasta)
      -Maharage(beans)
      -Ugali
Hivi ni baadhi ya vyakula wanavyokula wafuga rasta wasio kula nyama hata kile kinachodhalishwa na mnyama.....!!
  MWISHOOOOO
Kama kuna swali ruksa uliza..........!!!!!!!!!!!!
AHSANTENI SANA WADAU WANGU.............!!!!!!!!
NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA MWAKA MPYA...............!!!!!!!!!!!!
 BY IRON CHEF JACKSON


  



Saturday 28 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA KACHUMBALI YA MATUNDA(FRUITS SALAD)


         MAHITAJI
  -Ndizi(banana)
  -Embe(mango)
  -Nanasi(pineapple)
  -Machungwa(orange)
  -Sukari(sugar)
  -Maji(water)

     HATUA ZA KUANDAA
 -Weka sufuria yako jikoni pamoji na maji na sukari yako, acha mpaka ichemke na iyeyuke sukari, baada ya kuyeyuka sukari yako ipua sufuria yako na uhifadhi hayo maji katk bakuli na uweke katk friji yako huo mchanganyiko unaitwa(syrup).
 -Katakata matunda yako yote kwa mkato wa pembe nne(cubes) ila ukiwa unakata hakikisha tunda la liwe ni ndizi (banana), baada ya hapo weka katika bakuli lako.
 -Baada ya kukatakata matunda yako yote chukua ule mchanyiko wako wa maji na sukari(syrup) na uchanganye pamoja , baada ya hapo weka ktk friji tena mpaka chakula chako kitapokuwa tayari na userve pamoja.....!!!!
  
NAKUTAKIA KACHUMBALI NJEMA..............!!!!!!!!!!!
 HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA............!!!!!!!!!!!
 AHSANTENI SANA WADAU WANGU.............!!!!!!!!!!!!!!!
 BY IRON CHEF JACKSON










































Sunday 22 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA KUSAGA PAMOJA NA UNGA WA MIKATE(MASHED POTATO WITH BREAD CRUMB)

 Mahitaji
    -Viazi mbatata(mviringo)
    -Cream au maziwa
    -Spreadable cheese(philadelphia)
    -Kitimiri(coriender)
    -Majani ya laurusi (bay leaves)
    -Mayai
    -Unga wa ngano
    -Unga wa mikate

         Jinsi ya kuandaa sasa
    -Menya viazi na uvikate kate
    -Chopchop kitimiri(coriender)
   
          Hatua za kupika
    -Chemsha viazi,chumvi pamoja na majani ya laurusi(bay leaves), chemsha mpaka vilainike ili uweza kuviponda kwa baadae. Baada ya kuiva kwa viazi viipue na kuchuja maji na hatimaye weka sufuria yako tena jikoni na uweke viazi vyako ambavyo ulivichuja hapo awali.Na uanze kuvisaga sasa.
    -Wakati unaendelea kuvisaga viazi vyako unatakiwa kuweka sasa Cream au maziwa,Spreadable cheese pamoja na kitimiri(coriender) huku unaendelea kuvisaga viazi yako.
    -Endelea kusaga viazi vyako kwa muda wa dakika 5, na hatimaye vitakuwa vimesagika na kuiva kabisa.
    -Baada ya hapo chukua viazi vyako na utengeneze shepu kama kibomba.
    -Baada ya hapo pasua mayai yako na uweke katika bakuli kubwa kidogo, na uweka unga wa ngano ktik bakuli yake kubwa nayo pamoja na unga wa mikate nayo .
    - Baada ya kutengeneza shepu yako kama ya kibomba, chukua sasa na uweke katk unga wa ngano, na uweke katika mayai na mwisho katika unga wa mikate na uifadhi pembeni utafanya hivyo mpaka utakapo maliza viazi kwa jinsi ulivyo vishepu umetoa vingapi.
   -Weka flampeni yako jikoni na mafuta kiasi ili ukaange sasa(shallow fry)   
   -utakaanga mpaka utapoona rangi ya brown.
   -Na hapo vitakuwa tayari unaweza ukala na sosi (sauce) yako.
 NAKUTAKIA CHAKULA CHEMA MPENDWA WANGU.........!!!!!!!!
 AHSANTENI SANA WADAU WANGU.............!!!!!!!!!
Hapa vikiwa katika unga wa mikate
Hapa umetengeneza ktk shepu na umeweka ktk mayai

 BY IRON CHEF JACKSON
   

Hapa unakaanga sasa
Hapa tayari kwa kuliwa sasa

Wednesday 18 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA WALI WA MAYAI KWA STAILI YA KICHINA( FRIED RICE CHINESS)

            MAHITAJI
  -Mchele
  -Mafuta( vegetable oil)
  -Soy sauce
  -Chumvi (salt)
  -Pilipili hoho (green pepper)
  -Karoti (carrot)
  -Maji ya moto (hot water0
  -Kuku(fillet chicken or breast chicken)
  -Vitunguu (onions)
  -Mayai
  - Siagi au blue band

                        HATUA ZA KUPIKA 
   -Diboni kuku wako( ondoa mifupa na ubakiwe na steki tu ya kuku), na ukatekate mkato wa julieni.
   -Katakata pilipili hoho,Karoti kwa mkato wa julieni.
   -Chopchop vitunguu vyako vyote.
   - Kaanga mayai yako na ukate julieni.
   -Chemsha maji yawe yamoto na uweke pembeni.
   -Osha mchele wako na uweke pembeni.
   -Weka sufuria yako jikoni pamoja na mafuta yako. Baada ya mafuta kupata moto weka vitunguu vyako.
   Baada ya vitunguu kuiva, weka mchele wako na ukaange kwa muda kidogo na uweke chumvi.
   -Baada ya kuukaanga mchele wako, weka maji yako yale ya moto na uufunike sasa.
   -Wakati sufuria yako ipo jikoni, chukua flampeni yako na uweke siagi au blue band,
   - Baada ya kuyeyuka blue bandi yako au siagi yako, weka karoti, hoho pamoja na kuku wako ambao ulidiboni(fillet) na ukaange(shallow fry)  pamoja na uweka soy sauce yako.
   - Baada ya kuiva huo mchanganyiko wako(kuku, hoho na karoti) weka pembeni sasa.
   -Baada ya wali kukaribia kuiva changanya huo mchanganyiko wako wa (kuku, hoho na karoti) pamoja na mayai yako weka pamoja katika wali na uchanganyi pamoja ili uchanyike, baada ya hapo ufunike kwa muda kidogo na utakuwa umeiva 
   - Sasa chakula tayari kwa kuliwa na kwenda mezani sasa

NAWATAKIA CHAKULA CHEMA..........!!!!!!!
 AHSANTENI SANA WADAU WANGU.........!!!!!!!!
 NAWATAKIA PIA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA............!!!!!!!!

BY IRON CHEF JACKSON
MAYAI MKATO WA JULIENI
  
KUKU AMEKATWA MKATO WA JULIENI
KAROTI NA HOHO ZIMEKATWA MKATO WA JULIENI
CHAKULA TAYARI KWA KULIWA

Saturday 14 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA KEKI YA UNGA WA MAHINDI

                  MAHITAJI
   -Unga wa mahindi 250g
   -Unga wa ngano 200g
   -Sukari 250g
   -Baking powder 10g
   -Vanila essence 1 kijiko cha chakula
   -Eggs 9(75g)
   -Cream au maziwa
   -Siagi(butter)


              HATUA ZA KUPIKA 
   -Unga wa mahindi pamoja na unga wa ngano changanya pamoja na uchekeche.
   -Weka sukari pamoja na siagi na uchanganye pamoja na uiweke katika mashine ya kuchanganyia
   -Ya vunje mayai yako na uweke vanila yako katika maya.
   -Chukua unga wako uliouchekecha na uweka baking powder
   -Weka mayai yako ambayo ndani yake kuna vanila na uchanganye pamoja katika mchanganyo wako siagi na sukari ikiwa ndani ya mashine ya kusagia na baada ya kuchanganyika unatakiwa uutoe huo mchanganyiko wako katika mashine.
   -Chukua unga wako( unga wa mahindi+ unga wa ngano+Baking powder) na uweke kidogo kidogo katika mchanganyiko wako ule wa (Siagi, Sukari, Mayai ambayo ndani yake kuna vanila) huku unakoroga utaendelea hivyo mpaka utakapoona imekuwa nzito nzito.....!!
  -Baada ya hapo utandaze katika baking tray yako na uweke katika oveni yako
  -Utaona rangi yake na kuwa kama ya njano..........!!!!!!
  -MWISHOOOOOOOOOO

NAKUTAKIA KEKI NJEMA UONJAPO.........!!!!!!!!!!

AHSANTENI SANA WADAU WANGU..........!!!!!!!!!!!
  
BY IRON CHEF JACKSON
   


   

Thursday 12 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA SUPU YA DENGU

                         MAHITAJI

       -Unga wa dengu(Lentts flour)
       -Mchuzi wa kuku(Chicken stock)
       -vitunguu maji(onions)
       -vitungu swaumu(garlic)
       -Majani ya vitunguu(leaks)
       -Majani ya kitimiri(coriender)
       -Chumvi(salt)
       -Pilipili manga
       -Siagi
                    HATUA ZA KUPIKA
       -Katakata(chopchop) vitunguu, vitunguu swaumu, majani ya vitunguu,majani ya kitimiri.
       -Chukua unga wa dengu pamoja na mchuzi wa kuku(chicken stock) changanya pamoja na uupige na whipped wakati unauchanganya.
      -Weka sufuria yako jikoni pamoja na siagi
      -Baada ya siagi kupata moto weka vitunguu maji,majani ya vitunguu, vitunguu swaumu,pamoja na majani ya kitimiri na ivikaange pamoja mpaka vieve pamoja.
      -Baada ya kuiva hivyo viungo, weka ule mchanganyiko wako wa mchuzi wa kuku(chicken stock)pamoja na unga wa dengu.
Baada ya hapo, weka chumvi pamoja na pilipili manga na uiache kwa muda ili ichemke na upunguze moto wako.
 -Baada ya hapo unatakiwa uiblendi katika blenda
 -Endapo ikaonekana nzito sana unatakiwa uongeze mchuzi wa kuku(chicken stock) au maji.
Na hapo supu yako itakuwa imekamilika

NAKUTAKIA CHAKULA CHEMA

AHSANTENI SANA WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON
 Hapa imekwisha iva tayari













Hapa tayari kwa kuliwa kabisa

Sunday 8 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA PILAU YA NYAMA YA NG'OMBE

                     MAHITAJI
  -Mchele 
  -Nyama ya ng'ombe
  -Viazi mbatata(mviringo)(potato)
  -Vitunguu maji(onions)
  -Vitunguu swaumu(garlic)
  -Tangawizi iliyosagwa(ginger)
  -Karafuu(cloves)
  -Pilipili manga(Black pepper)
  -Chumvi(salt)
  -Binzari nyembamba nzima(cumin seed 1/2 kijiko cha cahi)
  -Binzari nyembamba ya kusaga 1 kijiko cha chai
  -Mafuta(vegetable oil)
  -Limao
  -Pilipili(chilli)
  -pilipili hoho(green pepper)
  -Nyanya(fresh tomato)

                               HATUA ZA KUPIKA
   -Katakata ya nyama yako kulingana na saizi uitakayo mwenyewe
   -Chemsha ya nyama yako na pia weka limao, Tangawizi pamoja na chumvi.
   -Wakati inaendelea kuchemka nyama yako, loweka sasa mchele wako katika maji.
   -Menya viazi vyako, pia katakata vitunguu vyako pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni kwa ajili         ya baadae
   -Weka sufuri yako jikoni na uweke mafuta yako ya kupikia,baada ya mafuta kupata moto weka vitunguu vyako ( na vitunguu maji) na uvikaange mpaka viwe rangi ya kawia(brown)
   -Baada ya hapo weka nyama yako nayo ikaange mpaka iwe rangi ya kawia (brown), baada ya hapo weka kitunguu swaumu na tangawizi tena kidogo na uikoroge vizuri na uiache ili ikaangike kwa muda wa dakika 2 au 3
-Baada ya hapo weka spices(viungo) ambavyo ni Binzari nyembamba ya unga, karafuu, amdalasini, hiriki, pilipili manga pamoja na viazi mbatata(mviringo),baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mchanganyiko huo mpaka uchanganyike vizuri 
-Baada ya hapo weka mchele wako na ugeuze geuze ili uchanganyike na viungo 
-Baada ya hapo weka chumvi kwa kiasi sana na uweka maji yako yale ya moto ya kutosha na ukoroge na baada ya hapo funika na uchemke kwa moto wa wastani.Pindi maji yanakaribia kukauka weka Binzari nyembamba nzima na ufunike uchemke mpaka maji ya kauke.Maji yakisha kauka ugeuze na ufunike mpaka uive
                     MAANDALIZI YA KACHUMBARI
  -Katakata vitunguu katika bakuli na uweke chumvi na maji na vioshe kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu na uvioshe mpaka chumvi itoke
 -Baada ya hapo osha nyanya, pilipili hoho na ukatekate slice nyembamba na uchanganye katika vitunguu pia kamulia limao  na uweke chumvi pia unaweza weka pilipili kama ukipenda..........!!!!!!!!!!!!

NAWATAKIA CHAKULA CHEMA...............!!!!!!!!

AHSANTENI SANA WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON


  
  
        

  

Thursday 5 December 2013

JINSI YA KUPIKA KUKU KWA NJIA YA KUOKA(BAKED CHICKEN)

Baada ya kuweka viungo vyote
                                                   Baada ya kuoka katika oveni
                                              Chakula tayari kwa kuliwa pamoja na wali

                               MAHITAJI
                 
            -Kuku vipande 8
            -Mchuzi mweupe au mvinyo mweupe( white stock or white wine) 1/3 kikombe
            -Chumvi pinch
            -Mafuta ya zeituni(olive oil)
            -Pilipili manga(Black pepper or White pepper)
            -Ndimu
            -Rosemarry(majani)

                                         JINSI YA KUPIKA
           HATUA
-Washa oveni yako 200 sentigrade
-Weka vipande vyako vya kuku katika treyi(baking tray) na uvipange
-Weka chumvi yako sasa
-Weka ndimu
-Weka mafuta ya zeituni
-Weka mchuzi mweupe au mvinyo mweupe(white stock or white wine)
-Weka pilipili manga
-Weka rosemary (majani) choped
-Sasa weka katika oveni yako kwa muda wa dakika 30 lakin baada ya muda itakupasa uwageuze
Baada ya kuwa tayari ni vyema ukala na wali
 NAWATAKIA CHAKULA CHEMA
Ahsanteni sana Wadau wangu





 

Wednesday 4 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA KARANGA ZA MAYAI

Hiki chakula ni kama kianzio kabla ya mlo kamili(starter),chakula hiki kimebeba wanga pamoja na proteni kwa sababu karanga ni jamii ya wanga na pia mayai yana proteni.

                                 JINSI YA KUPIKA KARANGA ZA MAYAI

       Mahitaji
  -Karanga 400gm
  -Sukari vijiko 2
  -Unga wa ngano 1/3 cup
  -chumvi pinch

       Hatua za kupika
  -Roweka karanga pamoja na chumvi baada ya hapo na uzikaushe si lazima kukausha
  -Changanya yai pamoja na sukari mpaka iwe nyeupe huo mchanganyiko wako
  -Weka karanga zako katika huo mchanganyiko wako
  -Weka ngano mpaka uone inanatanata
  -Weka mafuta jikoni na uanze kuzikaanga,mpaka uone rangi brown na uzitoe
  -Baada ya hapo ni tayari kwa kuliwa , ila ni vyema zaidi ukala pamoja na soda au juisi basi utajsikia burudani kabisa.....!!!!!
AHSANTENI SANA WADAU WANGU BY IRON CHEF............!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!



Tuesday 3 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA UGALI NGUVU

Ugali ni chakula cha asili ya Tanzania ambacho kinatokana unga wa mahindi. Pia chakula hiki kimebeba asilimia kubwa ya WANGA. Pia vyakula vyenye jamii ya wanga huleta faida nzuri mwilini kama vile;
kuupa mwili nguvu, kujenga mwili(shape of the body) n.k

                                          JINSI YA KUPIKA UGALI NGUVU

                Mahitaji
-Unga wa sembe(mahindi)
-Unga wa dona(sembe)
-Maji

                  Hatua za kupika
-Chukua unga wa sembe na unga wa dona changanya pamoja
-Weka sufuria jikoni pamoja na maji
-Chemsha maji kwa muda wa dakika 5 au mpaka maji yapate moto
-Korogea unga wako ambao ni  mchanganyiko wa sembe na dona
-Acha kwa muda kidogo ili uji uchemke 
-Baada ya uji kuchemka,anzaa kusonga ugali sasa
-Baada ya kuona umeshikamana vizuri basi ugali wetu utakuwa umeiva kabisa 
-Kama utapenda kuufanyia garnish(kukipamba chakula chako na kwenda mezani)
Hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa, pia ni vizuri ikaendana na kitoweo safi kama nyama choma(grilled beef),n.k
AHSANTENI SANA WADAU WA BLOG YANGU

     


       
   
        -

NINGEPENDA KUWAELEZEA JUU YA MDALASINI WADAU WANGU

Nawashukuru kwa kuniunga mkono na kushiriana nami katika maswala misosi , hivyo baadhi ya wadau wangu walipenda nielezee juu ya mdalasini.
    
                                      MDALASINI
Hiki ni kiungo kimojawapo katika mapishi tofauti tofauti kwa mfano pilau, chai hata pia katika mchuzi wa kawia(brown stock). Lakini mdalasini ni dawa kwa upande mwingine kwa upande wa wakina Baba, Kaka hii hutasaidia hasa katika kuuza ndoa zetu au kuimarisha ndoa zetu pia unaweza sema inaongeza nguvu za kiume. Lakini si mdalasini pekee yake lazima uchanganye na asali pamoja na chai basi ukichanganya hivyo vitu utapata dawa kamili ya kuuza ndoa yako mpenzi.
 
                                  FAIDA YA MDALASINI KATIKA CHAKULA

           -Huleta radha safi katika chakula
           -Huleta harufu safi katika chakula
           -Huvutia hamu ya kula chakula
           -Huongeza nguvu za kiume kwa wakina baba pamoja na waki kaka

Kama nilivyosema hapo awali kwamba mdalasini ukichanganya na asali pamoja na chai unapata dawa safi ambayo husaidia kutibu baadhi ya magonjwa kama vile 
      -Maumivu ya viungo vya mwili
      -Pia husaidia kukuza nywele kama mtu akiwa amenyonyokwa na nywele kichwani
      -Pia kama nivyosema hapo awali husaidia kuongeza nguvu za kiume

AHSANTENI SANA WADAU WANGU WOTE NAHITAJI SANA USHIRIKIANO WENU ......!!!!

Monday 2 December 2013

KARIBU TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA KUSAGA (MASHED POTATOES)

Viazi vya kusaga ni chakula kitamu sana ambacho kimebeba asilimia kubwa ni Wanga pamoja na Proteni, chakula hichi kinafaida kubwa katika miili yetu kama vile kujenga mwili(shape of the body), kuupa mwili nguvu(to be strong of the body).Pia chakula hichi huwa kina wafaa watoto wadogo miaka 2 na kuendelea , pia kina wafaa sana wakina mama wajazito pamoja na wazee kwa ajili ya afya zao ktk mili yao.
                     
                                 TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA SASA

          Mahitaji
    -Viazi mbatata(mviringo)
    -Cream au maziwa
    -Spreadable cheese(philadelphia)
    -Kitimiri(coriender)
    -Majani ya laurusi (bay leaves)

         Jinsi ya kuandaa sasa
    -Menya viazi na uvikate kate
    -Chopchop kitimiri(coriender)
   
          Hatua za kupika
    -Chemsha viazi,chumvi pamoja na majani ya laurusi(bay leaves), chemsha mpaka vilainike ili uweza kuviponda kwa baadae. Baada ya kuiva kwa viazi viipue na kuchuja maji na hatimaye weka sufuria yako tena jikoni na uweke viazi vyako ambavyo ulivichuja hapo awali.Na uanze kuvisaga sasa.
    -Wakati unaendelea kuvisaga viazi vyako unatakiwa kuweka sasa Cream au maziwa,Spreadable cheese pamoja na kitimiri(coriender) huku unaendelea kuvisaga viazi yako.
    -Endelea kusaga viazi vyako kwa muda wa dakika 5, na hatimaye vitakuwa vimesagika na kuiva kabisa. 
Hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa, pia chakula hiki kina faa kuliwa sana na nyama choma(Grilled beef) ....!!!!!! 
Nawatakia chakula chakula chema