Wednesday 4 December 2013

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA KARANGA ZA MAYAI

Hiki chakula ni kama kianzio kabla ya mlo kamili(starter),chakula hiki kimebeba wanga pamoja na proteni kwa sababu karanga ni jamii ya wanga na pia mayai yana proteni.

                                 JINSI YA KUPIKA KARANGA ZA MAYAI

       Mahitaji
  -Karanga 400gm
  -Sukari vijiko 2
  -Unga wa ngano 1/3 cup
  -chumvi pinch

       Hatua za kupika
  -Roweka karanga pamoja na chumvi baada ya hapo na uzikaushe si lazima kukausha
  -Changanya yai pamoja na sukari mpaka iwe nyeupe huo mchanganyiko wako
  -Weka karanga zako katika huo mchanganyiko wako
  -Weka ngano mpaka uone inanatanata
  -Weka mafuta jikoni na uanze kuzikaanga,mpaka uone rangi brown na uzitoe
  -Baada ya hapo ni tayari kwa kuliwa , ila ni vyema zaidi ukala pamoja na soda au juisi basi utajsikia burudani kabisa.....!!!!!
AHSANTENI SANA WADAU WANGU BY IRON CHEF............!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!



No comments:

Post a Comment