Thursday, 13 August 2015

KARIBUN TUJIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA MARBLE KAKE

Hii inaliwa na watu                   6 - 8
Muda wa maandalizi ni dakika      15
Muda wa kupika                             50


MAHITAJI
- Mayai 3
- Siagi 3/4 kikombe
- Chumvi pinch
- Unga wa ngano  1 -1/3 vikombe
- Baking powder 1 kijiko kimoja cha chai
- Sukari  1 kikombe
- Cocoa powder 1/2



JINSI YA KUPIKA

  1. Vunja mayai yako na utenge viini pamoja na utete, yeyusha siagi yako. Changanya utete wa mayai yako pamoja na chumvi na unachanganye vizuri, na baada ya hapo chukua unga wako wa ngano na uchangaye na baking powder pamoja.
  2. Chukua Siagi yako uliyeyusha na uchanganye na sukari yako, baada ya hapo changanya pamoja na viini vya mayai na uendelee kuchanganya.
  3. Chukua unga wako wa ngano ambao uliuchanganya pamoja na baking powder na uchanganye ktk ule mchanganyiko wako wa siagi, sukari na viini vya mayai.
  4.  Baada ya hapo changanya na ule uteute wa mayai ambao unamchanganyik wa chumvi u fold pamoja.
  5. Washa oven yako nyuzi joto 400F
  6. Chukua ule mchanganyiko wako na uugawe ktk sehem mbili,.
  7. Baada ya kugawa mchanganyiko ktk mabakuli, basi bakuli moja wapo changaya na cocoa powder.
  8. Baada ya hapo paka baking tray yako siagi kidogo
  9. Baada hapo weka mchanganyiko wako kwa awamu yaani, utaanzaa labda kuweka mchanganyiko ambao hauna cocoa powder kidogo ktk baking tray then utaweka na ule mchanyiko amabao hauna cocoa powder, hutafanya hivyo kidogo kidogo mpaka baking tray yako itakapo kuwa full na baking tray ni moja michanganyiko yote miwili ktk baking tray moja



KARIBUNI SANA 


BY 

IRON YOUNG CHEF JACKSON

Wednesday, 12 August 2015

                                        JINSI YA KUPIKA TOMATO SAUCE
- Hii ni sauce ambayo utokana na nyanya kupitia tomato sauce unaweza kudhalisha sauce mbali mbali kma vile
  - Chill sauce
  - Arrabiata sauce
  - Boleness sauce n.k


Mahitaji
- Nyanya
- Vitunguu maji
- Vitunguu swaumu
- Leeks
- Sukari kijiko cha kimoja cha chai
- Tomato paste
- Tangawizi
- Maji au vegetable stocka
- Mafuta ya kupikia
- Corriender
- Chumvi


                      JINSI YA KUANDAA
1: Osha nyanya zako na ukate kwa style uipendayo, na uweke kwenye chombo kisafi.
2: Osha vitunguu maji na uchopped pamoja na leeks
3: Blend vitunguu swaum pamoja na tangawizi
4: Chopped corriender(kotimiri)


                      JINSI YA KUPIKA

  1. Weka sufuria yako jikoni na uweke mafuta yako kidogo ya kupikia.
  2. Weka vitunguu maji pamoja na vitunguu swaum na tangawizi ulivyo blend na uweke na leeks pamoja na kotimiri
  3. Baada ya hapo weka nyanya zako na ukoroge koroge na uache mpaka nyanya ziive na uweke maji yako kiasi.
  4. Baada ya hapo uweka tomato paste yako, na uendelee kukoroga kidogo.
  5. Weka chumvi pamoja na sukari na ukoroge na uiche kwa muda wa dakika 5 na uzime ujiko.
  6. Baada ya hapo chukua na uiblend na huo mchuzi utakao patikan ndio sauce yenyewe.


NOTE
Kupitia sauce hiyo unaweza kupikia chakula chochote upendacho kam TAMBI, BEEF, CHICKEN, N.K



KARIBUNI SANA


BY

IRON YOUNG CHEF JACKSON


Thursday, 29 May 2014

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA NYAMA KWA MTINDO WA KICHINA( BEEF CHINESE STYLE)

       MAHITAJI
-Nyama (beef steak)
-Soy sauce
-Worcester sauce
-Vitunguu(onions)
-Vitunguu swaumu(garlic)
-Tangawizi(ginger)
-Pilipili hoho(green pepper)
-Karoti(carrot)
-Pilipili manga(black pepper)
-Chumvi(salt)
-Mchuzi wa kuku au mchuzi wa nyama au mvinyo mweupe(beef stock, chicken stock or white wine)
-Mafuta ya kula(oil)


      MAANDALIZI YA KUPIKA
-Katakata vitunguu, pilipili hoho na karoti kwa mtindo wa julieni.
-Katakata nyama pia kwa mtindo wa julieni.
-Saga tangawizi pamoja na vitunguu swaumu


      HATUA ZA KUPIKA
-Chemsha nyama
-Baada ya kuiva nyama yako ichuje na ule mchuzi wake weka pembeni
-Weka pan yako jikon na mafuta kidogo na baada ya mafuta kupata moto weka vitunguu maji, vitunguu swaumu, tangawizi na ukaange kwa dakika 3.
-Baada ya hapo weka karoti na pilipili hoho na ukaange kwa dakika 3 na uweke chumvi kidogo.
-Baada ya kuiva hizo mbogamboga weka pembeni pia.
-Baada ya hapo weka pan yako nyingine na uweke mafuta kidogo na uweke vitunguu, vitunguu swaum na tangawizi hivyo vyote weka kwakiasi kidogo.
-Baada ya hapo weka nyama na uikange kidogo na uweke mbogamboga zako, kwakuwa ulishazikaanga hapo awali zinapaswa zisiive san.
-Baada ya hapo weka soy sauce, Worcester sauce na ukologe.
-Baada ya hapo uweka stock yako yaani mchuzi wa kuku au mchuzi wa nyama ya uliohemshia au mvinyo mweupe
-Baada ya weka chumvi pamoja na pilipili manga

ANAGALIA BAADHI YA PICHA
.
























NAWATAKIA CHAKULA CHEMA

AHSANTENI WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON


Thursday, 22 May 2014

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA MCHELE WA BASMAT


        MAHITAJI
 
-Mchele wa basmat(basmat rice)
-Binzari(tumeric)
-Vitunguu(onions)
-Chumvi(salt)
-Maji(water)
-Mafuta ya kura


                 HATUA ZA KUPIKA
-Osha mchele kwa maji mara moja tu
-Weka sufuria pamoja na maji
-Baada ya maji kuchemka weka chumvi pamoja na mchele
-Wakati unauchemsha unatakiwa usiive sana maana utakuwa kama uji(bokoboko)
-Baada ya hapo uchuje mchele na uweke pembeni
-Chukua sufuria yako na uweke mafuta
-Baada ya weka vitunguu vyako ambavyo utakuwa umekata mtindo wa chopchop
-Baada ya vitunguu kuiva weka binzari yako pia na uendelee kukologa ili isishikane
-Baada ya hapo, weka mchele wako ktk sufuri yako yenye vitunguu na binzari
-Baada ya hapo endelea kukologa ili uchanganyikane na viungo
-Baada ya hapo zima jiko na chakula kitakuwa tayari
-Chukua pani yako na uweke mafuta mengi kwa ajili ya kukaanga vitunguu ambavyo utakuwa umekata kwa mtindo wa nusu duara(half ring) na uanze kuvikaanga mpaka upate rangi ya kahawia(brown).
-Baada ya hapo pakuwa wali wako ktk bakuli kubwa na juu yake uweke vitunguu ulivyokaanga
- Hapo chakula tayari kwa kuliwa

NAWATAKIA CHAKULA CHEMA WADAU WANGU

AHSANTEN SANA WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON









Monday, 17 February 2014

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA MCHUZI WA NYAMA AU BEEF STEW

           
                  MAHITAJI
        - Nyama ya ng'ombe (Beef)
        - Soy sauce
        -Vitunguu (onions)
        -Mafuta ya kula( vegetable oil)
        -vitunguu swaumu(garlic)
        - Pilipili hoho(green pepper)
        - Karoti(carrot)
         -Pilipili manga(black powder)
         - mchuzi wa nyama(beef stock or beef broth)
         -Nyanya ya kusaga(Tomato paste)


                   HATUA ZA KUPIKA
          -Katakata nyama kwa mkato wa pembe nne(cubes)
         - Chemsha nyama yako mpaka iive kabisa na vitunguu swaumu
         -Katakata karoti, pilipili hoho, pamoja na vitunguu kwa mkato wa julieni
         -Baada ya nyama yako kuiva weka pembeni na uweke flampeni weka mafuta kiasi kidogo sana
         - Baada ya mafuta kupata moto weka vitungu, pilipili hoho pamoja na karoti na uanze kuangaa(sautee)
         -Wakati naendelea kukaanga weka soy sauce
         -Baaada ya kuiva mbogamboga zako(karoti, vitunguu na pilipili hoho) ipua na uweke pembeni
         -Baada yapo chukua nyama yako ambayo uliichemsha na uichuje na ule mchuzi wako utunze kwaajili              ya baadae.
         -Baada ya hapo chukua nyama flampeni na uweke mafuta kidogo na uikaange
         - Baada ya hapo weka zile mbogamboga zako(karoti, pilipili hoho na vitunguu) yaani uchanganye                     pamoja na nyama yako
         -Baada ya kuchanya mbogamboga zako, weka soy sauce
         -Baada ya hapo weka nyanya yako ya kusaga(tomato paste) na uikologe au kuichanganya pamoja
         - Baada ya weka mchuzi wako uliouchuja kutoka ktk nyama, au mchuzi wa nyama(beef stock or broth
         - Baada ya hapo weka pilipili manga,na chumvi(black pepper and salt)
         -Baada ya hapo punguza moto wako na uiache kwa muda wa dakika 5 tu na uipue
         - Chakula hichi unaweza ukala na wali(rice)
         -Mwishooooooooo

AHSANTEN SANA WADAU WANGU.........!!!!!
 NAWATAKIA CHAKULA CHEMA WAPENDWA............!!!!!!!


ANGALIA HII PICHA...!!!!













 


       

Monday, 30 December 2013

JE UNAJUA VYAKULA GANI WANAOKULA WAFUGA RASTA(DO YOU KNOW THE KIND OF FOODS WHO ARE EATING VEGETARIAN)

                                WAFUGA RASTA(VEGETARIAN PEOPLE)
Hawa ni watu ambao wasio kula nyama ya aina yeyote, kutoka na imani walizonazo kwa mfano, imani za kidini kwa wenzetu wahindi huwa hawali nyama ya ng'ombe wakiamini ndie muumba wao, pia wat hawa huwa hawapendi wakimuona myama anachinjwa au kuona damu ya mnyama.

                                       AINA ZA WAFUGA RASTA
   Hawa wafuga rasta wamegawanyika katika makundi mawili(2) ambayo ni
        -Kuna wafuga rasta wasio kula nyama kabisa
        -Kuna wafuga rasta wasio kula nyama na hata kile kinachodhalishwa na mnyama .

                         WAFUGA RASTA WASIO KULA NYAMA
Hili ni kundi la wafuga rasta wasio kula nyama kabisa, hivyo kundi hili huwa wanakula vyakula vinavyodhalishwa na mnyama kwa mfano, maziwa, mayai n.k 

       AINA ZA VYAKULA WANAVYOKULA WAFUGA RASTA WASIO KULA NYAMA
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula wanavyokula wafuga rasta wasiokula nyama tu, ambayo ni
        -Maziwa(milk)
        -Mayai(eggs)
        -Mbogamboga za majani(vegetables)
        -Tambi(pasta)
        -Wali(rice)
Hivyo ni baadhi ya vyakula wanavyokula kundi hili la wafuga rasta wasio kula nyama.

WAFUGA RASTA WASIO KULA NYAMA HATA KINACHODHALISHWA NA MNYAMA
Hili ni kundi la wafuga rasta ambalo hawali nyama wala anachaodhalisha mnyama kwa mfano nyama, mayai, maziwa n.k hivyo vyakula jamii ka hii huwa hawali kabisa.

AINA ZA VYAKULA WANAVYOKULA WAFUGA RASTA WASIOKULA NYAMA HATA KINACHODHALISHWA NA MNYAMA
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula wanavyokula aina hii ya wafuga rasta ambavyo ni
      -Mbogamboga za majani(vegetable)
      -Wali(rice)
      -Tambi(pasta)
      -Maharage(beans)
      -Ugali
Hivi ni baadhi ya vyakula wanavyokula wafuga rasta wasio kula nyama hata kile kinachodhalishwa na mnyama.....!!
  MWISHOOOOO
Kama kuna swali ruksa uliza..........!!!!!!!!!!!!
AHSANTENI SANA WADAU WANGU.............!!!!!!!!
NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA MWAKA MPYA...............!!!!!!!!!!!!
 BY IRON CHEF JACKSON