Thursday 22 May 2014

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA MCHELE WA BASMAT


        MAHITAJI
 
-Mchele wa basmat(basmat rice)
-Binzari(tumeric)
-Vitunguu(onions)
-Chumvi(salt)
-Maji(water)
-Mafuta ya kura


                 HATUA ZA KUPIKA
-Osha mchele kwa maji mara moja tu
-Weka sufuria pamoja na maji
-Baada ya maji kuchemka weka chumvi pamoja na mchele
-Wakati unauchemsha unatakiwa usiive sana maana utakuwa kama uji(bokoboko)
-Baada ya hapo uchuje mchele na uweke pembeni
-Chukua sufuria yako na uweke mafuta
-Baada ya weka vitunguu vyako ambavyo utakuwa umekata mtindo wa chopchop
-Baada ya vitunguu kuiva weka binzari yako pia na uendelee kukologa ili isishikane
-Baada ya hapo, weka mchele wako ktk sufuri yako yenye vitunguu na binzari
-Baada ya hapo endelea kukologa ili uchanganyikane na viungo
-Baada ya hapo zima jiko na chakula kitakuwa tayari
-Chukua pani yako na uweke mafuta mengi kwa ajili ya kukaanga vitunguu ambavyo utakuwa umekata kwa mtindo wa nusu duara(half ring) na uanze kuvikaanga mpaka upate rangi ya kahawia(brown).
-Baada ya hapo pakuwa wali wako ktk bakuli kubwa na juu yake uweke vitunguu ulivyokaanga
- Hapo chakula tayari kwa kuliwa

NAWATAKIA CHAKULA CHEMA WADAU WANGU

AHSANTEN SANA WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON









No comments:

Post a Comment