Thursday 29 May 2014

KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA NYAMA KWA MTINDO WA KICHINA( BEEF CHINESE STYLE)

       MAHITAJI
-Nyama (beef steak)
-Soy sauce
-Worcester sauce
-Vitunguu(onions)
-Vitunguu swaumu(garlic)
-Tangawizi(ginger)
-Pilipili hoho(green pepper)
-Karoti(carrot)
-Pilipili manga(black pepper)
-Chumvi(salt)
-Mchuzi wa kuku au mchuzi wa nyama au mvinyo mweupe(beef stock, chicken stock or white wine)
-Mafuta ya kula(oil)


      MAANDALIZI YA KUPIKA
-Katakata vitunguu, pilipili hoho na karoti kwa mtindo wa julieni.
-Katakata nyama pia kwa mtindo wa julieni.
-Saga tangawizi pamoja na vitunguu swaumu


      HATUA ZA KUPIKA
-Chemsha nyama
-Baada ya kuiva nyama yako ichuje na ule mchuzi wake weka pembeni
-Weka pan yako jikon na mafuta kidogo na baada ya mafuta kupata moto weka vitunguu maji, vitunguu swaumu, tangawizi na ukaange kwa dakika 3.
-Baada ya hapo weka karoti na pilipili hoho na ukaange kwa dakika 3 na uweke chumvi kidogo.
-Baada ya kuiva hizo mbogamboga weka pembeni pia.
-Baada ya hapo weka pan yako nyingine na uweke mafuta kidogo na uweke vitunguu, vitunguu swaum na tangawizi hivyo vyote weka kwakiasi kidogo.
-Baada ya hapo weka nyama na uikange kidogo na uweke mbogamboga zako, kwakuwa ulishazikaanga hapo awali zinapaswa zisiive san.
-Baada ya hapo weka soy sauce, Worcester sauce na ukologe.
-Baada ya hapo uweka stock yako yaani mchuzi wa kuku au mchuzi wa nyama ya uliohemshia au mvinyo mweupe
-Baada ya weka chumvi pamoja na pilipili manga

ANAGALIA BAADHI YA PICHA
.
























NAWATAKIA CHAKULA CHEMA

AHSANTENI WADAU WANGU

BY IRON CHEF JACKSON


No comments:

Post a Comment