Monday, 17 February 2014
KARIBUNI TUJIFUNZE JINSI YA KUPIKA MCHUZI WA NYAMA AU BEEF STEW
MAHITAJI
- Nyama ya ng'ombe (Beef)
- Soy sauce
-Vitunguu (onions)
-Mafuta ya kula( vegetable oil)
-vitunguu swaumu(garlic)
- Pilipili hoho(green pepper)
- Karoti(carrot)
-Pilipili manga(black powder)
- mchuzi wa nyama(beef stock or beef broth)
-Nyanya ya kusaga(Tomato paste)
HATUA ZA KUPIKA
-Katakata nyama kwa mkato wa pembe nne(cubes)
- Chemsha nyama yako mpaka iive kabisa na vitunguu swaumu
-Katakata karoti, pilipili hoho, pamoja na vitunguu kwa mkato wa julieni
-Baada ya nyama yako kuiva weka pembeni na uweke flampeni weka mafuta kiasi kidogo sana
- Baada ya mafuta kupata moto weka vitungu, pilipili hoho pamoja na karoti na uanze kuangaa(sautee)
-Wakati naendelea kukaanga weka soy sauce
-Baaada ya kuiva mbogamboga zako(karoti, vitunguu na pilipili hoho) ipua na uweke pembeni
-Baada yapo chukua nyama yako ambayo uliichemsha na uichuje na ule mchuzi wako utunze kwaajili ya baadae.
-Baada ya hapo chukua nyama flampeni na uweke mafuta kidogo na uikaange
- Baada ya hapo weka zile mbogamboga zako(karoti, pilipili hoho na vitunguu) yaani uchanganye pamoja na nyama yako
-Baada ya kuchanya mbogamboga zako, weka soy sauce
-Baada ya hapo weka nyanya yako ya kusaga(tomato paste) na uikologe au kuichanganya pamoja
- Baada ya weka mchuzi wako uliouchuja kutoka ktk nyama, au mchuzi wa nyama(beef stock or broth
- Baada ya hapo weka pilipili manga,na chumvi(black pepper and salt)
-Baada ya hapo punguza moto wako na uiache kwa muda wa dakika 5 tu na uipue
- Chakula hichi unaweza ukala na wali(rice)
-Mwishooooooooo
AHSANTEN SANA WADAU WANGU.........!!!!!
NAWATAKIA CHAKULA CHEMA WAPENDWA............!!!!!!!
ANGALIA HII PICHA...!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment